"Mpaka sasa miezi imeanza kuhesabika huku bendi ikiwa katika hatua zingine za mabadiliko hali inayofanya mashabiki kuona tofauti kubwa yenye tija katika uongozi mpya wa Zagreb ,"alisema Rama.
Rama alisema kuwa kumekuwa na mambo muhimu katika ujio wake kiuongozi na hivyo hali hiyo inachochea mashabiki pia kuona badiliko katika bendi.
Kwa sasa bendi hiyo ambayo ni kati ya bendi zenye ushindani mkubwa nchini tangu mwishoni mwa mwaka jana inaonesha kuwa na mabaliko hayo makubwa kwa mashabiki wake na imekuwa ikifanya vyema katika Bonanza lake la kila Jumapili Msasani Beach Club.
Comments