Na Francis Peter
SUALA la Udjs kwa sasa limeishakuwa zaidi ya ajira kutokana na ufanyaji wa hatua za
masuala hayo kuendelea zaidi katika maeneo mengi yenye tija za kuingiza kipato.
Awali miaka ya nyuma tena wakati mwandishi wa makala hii nikiwa katika hali ya udogo wa umri miaka ya nyuma nilikuwa nikioneshwa na jamaa walioku wamenitangulia pindi ma Djs hao walipokuwa katika pita pita zao mitaani.
Kadri nilivyo zidi kukua nikaanza kidatocha kwanza ndipo nilipoakuwa nawaona
zaidi kwa kwenda kwenye kumbi zao walipokuwa wakiporomosha nyimbo kuwapa raha mashabiki wa muziki wa Disco.
Taratibu miaka ilipoanza kusogea madjs waliokuwa wakichengua katika kumbi za Disco
wakanza kupata mashavu katika kuendesha vipindi mbali mbali vya muziki redioni na baada ya muda ikaanza kuwa ajira sahihi kwa kupata mikataba ya kiutumishi katika redio mbali mbali mbali kwa kwa kutumikia vipindi hivyo vya redio.
Moja ya Dj wenye majina katika jiji la Dar es Salaam Chande Mohamed 'Dj Q' ni moja
ya waliopitia katika ajira za redio nakufanya poa sana katika vipindi vya muziki kipindi cha miaka ya sasa aliweza kuendesha vipindi vya muziki Magic FM ambapo kwa sasa yeye ni moja ya watu wanaotengeneza ajira za watu wengine .
Mbali na kuanza kujiingizia kipato kwa kuthubutu kuandaa matamasha ya wanamuziki
wa Bbongoflava nchini katika kipindi cha miaka ya 2000 kuja juu sasa ni Boss wa Club 601 (Top Garage) iliyopo Tanki Bovu Mbezi Beach.
"Nimeweza kuendesha Disco langu nikiwa kama Boss wa ukumbi huu maisha yanaenda yanabadilika ni moja ya hatua zangu za kimafanikio katika maisha yangu nimeweza kuacha ajira na kujiajili na nimeweza tayari kutengeneza ajira kwa watu wengine kupitia
Club 601,"anasema Dj Q.
Boss huyo wa Club 601 Dj Q ambaye kwa sasa ameweza kugawa ajira kwa wengine ni kielelezo tosha cha ma Dj wengine kuweza kufikia malengo yao makubwa kwa kuwa wajasilia mali kama unavyo weza kuona ukiwa katika club yake hiyo Q.
Ukifika katika Club 601 unaweza kuburudishwa na muziki wa Disco kwa umahiri kufuataia nyimbo zinazopigwa katika mpangilio sahii uku ukiziona ajira alizo zitengeneza
Dj Q , utaona wahudumu wenye kujali mteja (weiters), na baadhi ya kaunta za kisasa
zitakazokufanya uendelee kuburudika na kufanya akili iweze kutulia kwa kiasi kikubwa.
"Maisha ni ubunifu (skills) za maisha unayoyapitia zinaweza kukujenga kupata muonekano bora wa kimaisha katika siku za usoni najihisi nafaidi najisiki nipon Okay katika hali niliyofikia kwa sasa ila bado napambana kwani namajukumu mengine ya kifamilia pia,"anasema Dj Q kwa ujasiri .
Udjs kwa unamvuto kwani maisha ya vijana wengi wanaofanya udj wamo katika ajira sehemu mbali mbali kuanzia kwenye kumbi kubwa za starehe kama Club Billicana na Club 601 pamoja na maeneo ya klabu zingine zimeweza kuajiri vijana na hivyo kuwapa maisha mazuri.
Anga za udjs katika miaka ya nyuma sana ilikuwa ni sifa tu kwa kijana
kuwa Dj na kupita mitaani wakinyooshewa vidole na kuonekana kupendwa
zaidi na mabinti lakini taratibu zama hizo zikafutika sasa
wanajichukulia mkwanja wa kutosha na nje ya kunyooshewa vidole vya sifa
pindi wanapo pita katika maeneo mbali mbali.
Dj Q amekuwa ni miongoni mwa madj wanaofunga zaidi kwa kupata nyomi la
mashabiki kuanzaia siku za Jumatano mpaka Jumapili kupitia Club 601
lakini ukitaka kwenda katika kiota hicho makamuzi yapo mkila siku mbali
na siku nilizozitaja hapo juu.
"Nawakaribisha sana vijana na watu wa miaka ya nyuma kwani nimekuwa
nikipiga kwa aina ya kipekee muziki wa (olds School) nakufanya furaha
yao kuwa kubwa kwa kuwakumbusha nyimbo za enzi zao ,"anamaliza kusema Q.
Comments