Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas
kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzia leo Aprili
27, 2016.
Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika
Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe
ya Usajili (TMS).
Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.
Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha.
Mawasiliano ya Afisa Habari,
Comments