Msanii mkongwe katika mziki wa bongo Q chief anaamini wingi wa
wasanii wanaosimamiwa na QS Entertainment unachelewesha mipango yake
kutimia.
Akiongea na Enewz ya EATV, Q chief amesema label hiyo ambayo ipo
chini ya QSJ Mhonda inasimamia wasanii wengi kiasi cha kuweka ugumu
kwenye mipango yake kutimia.
Hivi karibuni, Pia Q chief aliiambia Bongo5 kuwa bosi wake amekuwa mzito katika maamuzi mbalimbali ya kazi.
label hiyo inamsimamia Q chief, Mb dog, Bushoke, ina bendi ‘QS
International Band’ na pia label hii inamiliki wasanii wengine wachanga
kwa lengo la kuendeleza vipaji vipya.
Comments