April
19 2016 wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho
barani Africa (CAF) klabu ya Azam FC ilishuka mjini Rades
Tunisia kucheza mchezo wake wa marudiano wa Kombe la
shirikishoa barani Afrika dhidi ya klabu ya Esperance ya Tunisia.
Azam
FC ambao mchezo wa awali uliochezwa Chamazi
Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 2-1, wamekubali kipigo cha goli
3-0 katika mchezo huo wa marudiano. Kabla ya mchezo huo Azam FC walikuwa
wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze kusonga mbele. Magoli ya
Esperance yalifungwa na Bguir, Jouini na Errouge.
Baada ya
kuondolewa katika michuano kwa klabu ya Azam FC, Tanzania
inabakia na muwakilishi mmoja pekee katika michuano ya kimataifa, ambaye
ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans ambayo April 20 itacheza
mchezo wake wa marudiano na wenyeji wake Al Ahly.
Comments