Wakati wanyange wanaosaka kinyang'anyio cha kulitaka taji la ulimwende la Miss Dar City centre 2016 wakiwa wameanza kukutana kuanzia mwanzo mwa wiki hii kwenye ukumbi wa Club Maisha uliopo Kijitonyama Jijini hapa es Salaam kampuni ya uuzaji wa nywele bandia nchini Prima Afro Total Hair Collection ambao wanapatikana mtaa wa Narung'ombe, Kariakoo, Dar es Salaam wamejitokeza kudhamini shindano hilo .
Wauzaji hao wa nywele bandia ambao bidhaa zao zinapatikana nchi nzima ambapo kwa djijini Dar es Salaam wanapatika katika maduka yao yaliyopo Karia Koo,wamekuwa ni wauzaji wanaojihamini kumpendezesha mwanamke wa kisasa kuwa na mtazamo mkubwa kulingana na mwanamke anayekuwa ametumia bidhaa zao .
Kujitokeza kudhamini kwa wadhamini hao mwaka huu maandalizi ya shindano hilo tayari yameanza katika sehemu mbali mbali nchini mratibu wa shindano la Miss dar City centre 2016 Nancy Joseph anasema kuwa tayari wameanza maandali ya Shindano hilo ambapo wameanza kuwapokea washiriki wenye sifa hozo.
"Wiki hii tumeanza mchakato wa kuanza kuwapata mabinti wanaotaka kuchuana kumpata Miss dar City centre mwaka huu ambapo wanatakiwa kufika Club Maisha Kijitonyama , tunaomba warembo wafike kwa wingi kwani vigezo vya kujiunga na mazoezi wataambiwa mara watakapofika ,"anasema Nancy .
Nancy anasema kuwa tayari waishatafuta wadhamini wa shiondano hilo na baadhi ya wadhamini tayari wameahidi kudhamini shindano .
Hata hivyo wadhamini wa shindano la Miss dar City centre 2014 Prima Afro Total Hair Collection wamesema shindano hilo kawaida huwa ni lenye mafanikio lilikuwa na mafanikio katika wakati wa msimu uliopita mwaka 2014 ambapo tulijitokeza kudhamini kwa mara ya kwanzambapo kwa sasa pia tayari tumejitokeza tena.
Afisa masoko wa kampuni hiyo ya uuzaji wa hao wa nywelekwa mujibu wa Idd Gumbwe anasema bidhaa zao ni bora na zinahusu uzuri wa mwanamke na kwa kuwa bidha zao ni bora wanaamini kuwa watanogesha shindano hilo kwa warembowa shindano hilo .
Idd anasema kuwa mara nyingi mashindano hayo yamekuwa na hali ya kipekee katika kuwa na mvuto kwa jamii hivyo walijitokeza kudhamini shindano hilo kama sehemu ya kujitoa kwa kampuni yao kwa jamii na hatimaye mshindi Jihan Dimechk kutangazwa na kutwaa taji la Miss dar City centre 2014 .
Miss dar City centre ni moja ya shindano bora katika shindano la Miss Tanzania kwani limekuwa likitoa wanyange bora kabisa na mara kwa mara wameweza kutikisa katika kumi bora za kitaifa za shindano hilo.
Miss Dar City Centre linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi hii, Aprili 23 ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip City Center Jijini Dar , ukiwa ni ufunguzi maalum kwa ajili ya kuelekea katika shindano lenyewe litakalofanyika Mei 21, mwaka huu.
Naye msimamizi mkubwa wa shindano hilo Eric Janguo naye alipambanua kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kupata warembo wenye vigezo vingi watakao weza kufanya vyema katika shindano hilo hadi ngazi ya taifa.
Badhi ya wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini ni Golden Tulip City Center Jijini Dar es Salaam,Maji ya Zan Aqua , Tv 1, EML M&J Printing, Super Model Collections .
Comments