Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiongea na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania waliomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja mara baada ya kikao chao ljana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene amekutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na kupata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kushirikiana nao katika kutatua kero hizo.
Akizungumza na wafanyabiashara hao waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wamejadiliana masuala mbalimbali ya kibiashara ili yaweze kunufaisha jamii na taifa.
“Nimesikia mapendekezo yenu nitayafanyia kazi, nitawaita ili tujadiliane katika kujenga mazingira bora na rafiki ya biashara yatakuwa na manufaa kwenu taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Simbachawene.
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kushirikiana na wafanyabiashara nchini na kulihakikishia taifa kuwa uchumi imara kulingana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Katika kikao hicho wafanyabiashara walipata nafasi ya kumueleza Mhe. Waziri kero mbalimbali zinazowakabili zikiwepo utitiri wa kodi, ugumu katika upatikanaji wa leseni na kukosekana kwa uwiano wa tozo za leseni kati ya sehemu moja na nyingine ambapo Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi kero na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara waliyowasilisha kwake.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja alisema wafanyabiashara wanapenda kuona Tanzania ikikua kiuchumi na wao kama wafanyabiashara wangependa kuwa wadau wa kuisaidia nchi kukua kiuchumi, hivyo wanaomba serikali iweze kuwashirikisha katika masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kibiashara ili waweze kutoa mchango wao wa mawazo na kuondoa ugomvi kati ya wafanyabiashara na Serikali yao.
Miongoni mwa masuala ambayo Jumuia ya Wafanyabishara Tanzania imependekeza yaangaliwe kwa undani kuwa ni pamoja na serikali kuangalia upanuzi wa wigo wa ulipaji wa kodi,kuunganishwa kwa kodi na tozo mbalimbali katika ulipaji na kurahisishwa kwa utaratibu wa ulipaji wa leseni.
Comments