Mlinzi wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi amesifia kiwango cha mlinzi
mkongwe Oscar Joshua wa klabu hiyo ambaye wamekuwa wakichuana kuwania
nafasi katika kikosi cha kwanza, Mwinyi kwa sasa anauguza majeraha
ambayo yamemuweka nje ya uwanja na kumfanya akose michezo kadhaa ikiwa
ni pamoja na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly.
Mwinyi amesema Joshua ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya
kimataifa na amekuwa akicheza kabla hata yeye (Mwinyi) hajaanza kucheza
na alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wa marudiano ugenini dhidi
ya Alhly.
Abubar Kisandu amezungumza na mlinzi huyo wa kushoto wa Yanga na timu
ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambaye bado anaendea kuuguza majera
yake visiwani Zanzibar akiwa amepewa mapumziko ya muda.
“Kwanza mchezo ulikuwa mgumu kwasababu nyumbani tuli-draw kwahiyo
ugenini mchezo ulikuwa ni wa ushindani lakini timu yetu ilicheza
vizuri”, anasema Haji Mwinyi ambaye tangu atue Yanga amekuwa tishio kwa
nafasi ya Oscar Joshua ambaye mara nyingi amekuwa akianzia benchi.
“Sioni kama kuna pengo, Oscar Joshua alicheza vizuri kwasababu yeye
ni mzoefu kuliko hata mimi, yeye alianza kucheza kabla yangu na kwenye
mchezo dhidi ya Al Ahly alicheza vizuri sana”.
Comments