Maggid Mjengwa
Toleo la 451
30 Mar 2016
KASHFA ya baadhi ya wabunge wetu kupokea milungula ni jambo la aibu kwa taifa. Hii si mara ya kwanza, mwaka 2012, na kabla ya hapo ilitokea na niliandika kwenye safu hii. Kwamba Julius Kaisari alipata kutamka; “My wife ought not even to be under suspicion”- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.
Kaisari alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume cha mienendo mema ya ndoa.
Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari kumwacha mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa kutenda yalo maovu.
Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ile ya mwaka 2012 na hii ya sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba tulishuhudia mwaka 2012, kwa Waziri mwenye dhamana kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa , alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo. Ile ilikuwa ni kashfa kubwa. Si tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa nchi nzima. Na juzi hapa tumesikia wabunge wetu wakitokwa na mate kukimbilia milungula iliyopewa jina la ' lunch'.
Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hizi isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake itolewe kwa Bunge na umma.
Maana, hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari wameshajiuzulu.
Lakini, likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, waliotoa maelezo ya tuhuma hizo hadharani nao wanapaswa wajiuzulu mara moja na wachukuliwe hatua. Ni kwa vile, watakuwa wamesema uongo.
Na hayo yakifanyika, na kama..soma zaidi..

Comments