Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji la Dar es Salaam zimetakiwa kuondoka ifikapo Mei 2 Mwaka huu ilikupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi kuweza kufanya shughuli zake kuanzia hiyo Mei 10. Juzi, Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema mradi huo utaanza kutoa huduma kwa wakazi wa jiji hilo Mei 10.
Msemaji wa mradi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Dacoboa), Sabri Mabrouk alisema wamiliki wote wa daladala walilipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki wa mabasi walishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,’’ alisema.
Mabasi hayo zaidi ya 30 ya Darts yalianza kupita kwenye njia zote za mradi huo. Changamoto kubwa inayolalamikiwa ni muingiliano wa daladala, magari binafsi, pikipiki na raia kupita bila tahadhari kwenye njia za mradi.
Moja ya mabasi hayo jana lilipata ajali baada ya kukwaruzana na pikipiki eneo la Kinondoni.
“Nasikitika pikipiki zinapita wala madereva hawaangalii, wameshakwaruzana na basi la mradi, sijui itakuwaje mradi utakapoanza, elimu inahitaji kwa wananchi bila hivyo tutawapoteza wengi,” alisema Mabrouk
Alisema wamelazimika kufanya majaribio bila ya kubeba abiria kwa zaidi ya wiki kwa kuwa nauli mwafaka haijajulikana.Inatoka Mpekuzi
Comments