Mtangazaji wa redio Gardner G. Habash amerudi tena kufanya kazi na redio maarufu nchini Clouds Fm.
Habash ambaye alikuwa akifanya kazi Clouds Fm katika kipindi cha “Jahazi” alihamia redio ya Times Fm miaka miwili iliyopita.
Mume wa zamani wa mwanamuziki Lady JayDee amesaini mkataba mpya na redio hiyo yenye maskani yake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Gardner G. Habash ataungana tena na Emphraim Kibonde katika kipindi
cha “Jahazi” kinachorushwa siku za wiki kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 1
jioni Clouds Fm.
Comments