Kwa mara nyingine Nigeria Super Eagles watakosekana kwenye michuano
ya mataifa ya Afrika (African Nations Cup) kwa mara ya pili mfululizo
baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Misri kwenye mchezo wa
marudiano na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-1baada ya kucheza michezo
yote miwili.
Kwan nchi yenye wakazi wengi kuliku nchi nyingine za kiafrika, ambayo
inatoa wachezaji wengi kwenda nje ya Afrika na imekuwa juu ya soka la
Afrika kwa muda mrefu ni jambo la kushangaza kushuhudia Nigeria
ikianguka.
Kushindwa kufuzu kwa msimu huu kunaifanya kuyakosa mashindano hayo
kwa mara tatu ndani ya miaka minne. Hiyo inaonesha kwamba Nigeria
imekuwa kama chambo na kutokana na kiwango wanachokionesha wanatakiwa
kuangaliwa kama chambo kwenye soka la Afrika.
Kutambua tatizo ni hatua ya kwanza kuelekea kutauta ufumbuzi, na hapa ndipo Nigeria wanahitaji kuanzia:
- Kumwacha Samson Siasia aendelee kuwa kocha mkuu
Wakati matatizo yanaanza kwenye kikosi cha Nigeria, ilijikuta
kikaangoni pale iliposhindwa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika
mwaka 2012.
Badala ya kurudi nyuma kuangalia kwanini timu ilishindwa kufuzu na
kipi kilihitajika kufanywalakini haraka Siasia alitimuliwa kazi. Licha
ya kwamba kikosi cha wakati huo kilikuwa kikicheza soka la kuvutia,
kilikua pia kinafunga magoli ya kutosha.
Kipindi hiki cha kutafuta nafasi ya kufuzu kwa michuano ijayo,
makocha watatu wakiwa na style zao tofauti za ufundishaji na wamewaita
wachezaji tofautitofauti kila mmoja kwa kipindi chake. Kila kocha akija
na nahodha wake tofauti.
Siasia ameteuliwa kama kocha wa muda, lakini ni wakati sahihi chama
cha soka cha Nigeria (NFF) kumpa mkataba wa muda mrefu kuendeleza
harakati alizozianza.
Hakuna haja ya kocha mpya kuja tena na kuanza upya kwenye mchakato ambao tayari umeanza kupamba moto.
Tulichokiona kwenye dakika zaidi ya 180 dhidi ya Misri ni wachezaji
kucheza soka safi kitimu, kutengeneza nafasi, na kikaonesha kuwa
kitakuwa vizuri baada ya muda lakini kinaangushwa na safu ya ulinzi.
Wapewe muda na kwa msaada wa kiufundi wanaoupata kutoka kwa Shaibu
Amodu hii ni timu ambayo inaweza ikafika mbali kama wataamua kumpa muda
kocha.
- Soka lazima liwe huru
Ni rahisi kutupa lawama zote kwa NFF, kiungwana hiki ndiyo chombo
ambacho kinasimamia soka hivyo kinatakiwa kuwajibika. Nigeria imeshindwa
kufuzu chini ya uongozi wa makocha watatu tofauti ni kitu cha
kushangaza.
Serikali kuingilia shughuli za NFF inaweza ikawa sababu ya kushindwa
kufanya kazi zake vizuri. Kusubiri kwa miezi kadhaa kuhusu masuala ya
kifedha kukamilishwa hata baada ya bajeti kuwa iko wazi hii inaiathiri
timu kwenye maandalizi na mipango yake
- Wachezaji lazima waoneshe utayari wao
Siku za nyuma wakati Nigeria ikiwa ni timu tishio barani Afrika,
wachezaji wake hawakuwa wakicheza kwenye vilabu vikubwa vya Ulaya. Na
wakati huo kunawachezaji walikuwa hawana timu, walichokuwa wanakifanya
ni kujitoa na kupambana kwa ajili ya timu yao.
Na timu ya kipindi hicho ndiyo iliitambulisha The Super Eagles nje ya
mipaka ya Afrika. Wakati huo wachezaji walikuwa na uzalendo na
kujiamini na walikuwa wakionekana hivyo katikati ya uwanja.
Nigeria ilimtunza kocha na kumwachia majukumu ya kuijenga tofauti na
sasa ambapo wachezaji wamekuwa hawana uhakika kama wataitwa kwenye mechi
inayofuata au la.
- Kutengeneza mfumo utakaombeba Ighalo
Kwasasa striker wa Watford Odion Ighalo bila shaka ndiye mchezaji
hatari zaidi barani Ulaya. Ameweza kufunga magoli ya kutosha kwenye
Premier League lakini akiwa na Nigeria ameshindwa kufunga hata goli moja
kwenye michezo miwili na hapa ndipo maswali yanaweza kuibuka. Je watu
watilie mashaka kiwango chake? Au mfumo haumfanyi ang’ae?
Ushahidi ambao mtu anaweza kutoa kutokana na michezo hiyo miwili ni
kwamba, mfumo ndiyo tatizo. Kwa kipindi kirefu, Ighalo alionekana
pekeake akiwa katikati ya mabeki wawili akiwa hana msaada. Kuna wakati
alishuka chini na kuchukua mpira akaenda pembeni kisha akampigia pasi
Ahmed Musa ambaye alikuwa amesogea katikati ya uwanja lakini alishindwa
kuusoma mchezo huo na hakuukimbilia mpira.
Alicheza vizuri baada ya Alex Iwobi kuingia, kinda wa Arsenal mwenye
uwezo wa kukimbia na walikuwa wakibadilisha nafasi hali iliyowapa shida
mabeki wa Misri
Ni wakati muafaka sasa kwa Siasia kubadilisha mfumo ili uwafit
wachezaji anaowatumia. Mashabiki wengi tayari wameanza kumkosoa Ighalo
na litakuwa kosa kubwa kwa Siasia kumtema mchezaji huo.
Rashidi Yekini alipoteza nafasi kibao, lakini anajiamini kwasababu
anajua kwamba kocha na wachezaji wenzake wanaimani nae. Jambo hili pia
Ighalo anahitaji kuwanalo.
- Marekebisho kwenye safu ya ulinzi
Eneo la ulinzi lilitumika kama sehemu muhimu ya kikosi cha Nigeria.
Lakini miaka ya hivi karibuni kitu hicho hakipo kwenye kikosi hicho.
Stephen Keshi alijitahidi kuliziba pengo hilo kwa kucheza style ya
kuzuia ambayo ilikuwa haipendezi kuangalia japo ilimsaidia lakini bado
sehemu hiyo haijawa salama kwa muda sasa.
Siasia amekuwa na mfumo wa aina nyingine wa kushambulia. Ukifanikiwa
ni mfumo unaovutia lakini timu ikishindwa kufunga unakuwa hatari.
Comments