ligi kuu England iliendelea usiku wa Alhamis 21 April kwa
michezo mmoja ulio kati ya Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa
Emirate wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.
Mshambuliaji Alexis Sanchez ndie alikuwa shujaa wa mchezo huo baada
ya kuzipasia nyavu mara mbili alianza kufunga goli la kwa katika dakika
ya 6 ya mchezo kisha akifunga goli la pili kwa mpira wa adhabu katika
dakika ya 38.
Katika mchezo huo timu ya Arsenal iliutawala kwa asilimia 71, huku
West Brom wakiutawala kwa asilimia 29. Kwa ushindi huo vijana wa Profesa
Arsenal Wenger, wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa kwenye nne bora
baada ya kujikusanyia alama 63 katika michezo 34 waliyocheza.
Arsenal wamesaliwa na michezo minne mkono kabla ya kumalizika kwa ligi kuu England msimu
Comments