Kampuni ya rapa huyo wa Marekani Roc Nation Sports inasemekana imeanza kujenga uhusiano wa karibu na nyota huyo mwenye miaka 18.
Rashford ana magoli manne katika mechi saba za ligi alizocheza tangu
alipoingia kwenye kikosi cha kwanza Man United mwisho wa mwezi Februari
na aliwashusha daraja Aston Villa katika mechi iliyopigwa Jumamosi Old
Trafford.
Kwa mujibu wa The Sun, Roc Nation imefanya mazungumzo ya awali na familia ya Rashford kuhusu kumuingiza kwenye rosta ambayo yumo pia beki wa Bayern Munich Jerome Boateng na mwana masumbwi wa Marekani Andre Ward.
Rashford anatarajiwa kusaini mkataba mpya United majira ya joto ambao utaupandisha ujira wake hati paundi 15,000 kwa wiki.
Comments