Bw Ruto anataka kesi dhidi yake iondolewe
Makamu wa
Rais wa Kenya William Ruto atafahamu leo iwapo kesi inayomkabili katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) itatupiliwa mbali.
Mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, pia atafahamu leo iwapo ana kesi ya kujibu.
Bw Ruto
anakabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso
yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Amekana mashtaka hayo na mawakili wake wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.
Upande wa mashtaka umekabiliwa na changamoto kadha kwenye kesi hiyo dhidi yake.
Mwezi
Februari, majaji katika mahakama hiyo waliizuia afisi ya mwendesha
mashtaka kutumia ushahidi wa mashahidi ambao tayari wamejiondoa.
Mashahidi
kadha muhimu walibadilisha taarifa zao za ushahidi, jambo ambalo
waendesha mashtaka wanasema lilitokana na vitisho na kuhongwa.
Mawakili
wa Bw Ruto wanasema anafaa kuondolewa kesi hiyo kwa sababu mashahidi
wengi wa upande wa mashtaka wamejiondoa au wakabadilisha taarifa zao
asili za ushahidi.
- Ruto ashinda rufaa mahakama ya ICC
- Mashahidi wa Ruto katika ICC
- Bensouda:Sikabiliwi na shinikizo zozote
Mwendesha
mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda amekiri kwamba kujiondoa kwa
mashahidi kumeathiri kesi dhidi ya naibu huyo wa rais lakini anasisitiza
kwamba bado kuna ushahidi wa kutosha wa kuendelea na kesi hiyo. BBC
Comments