Beki
wa zamani wa Arsenal amekaa kwa muda wa siku 22 tu kwenye club yake ya
Sunderland na kufukuzwa kazi. Eboue ali sign mkataba wa muda mfupi na
club hiyo inayoshiriki EPL akiwa free agent.
Sababu ya msingi ni kwamba FIFA imemfungia Eboue kujihusisha na soka
kwa muda wa mwaka mmoja hadi pale atakampomlipa wakala wake wa zamani.
Kwenye adhabu hiyo FIFA wamesema anaweza kujihusha na soka kama akilipa
deni hilo.
Club ya Sunderland haikutaka la kusikia chochote baada ya adhabu
hiyo. Walichokifanya ni kumfukuza kazi kabisa Eboue. Pia hata kama
akimalizana na wakala wake bado hawana nafasi kwa ajili yake tena.
Comments