Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2016

Alfred Lucas Afisa Habari mpya TFF

Afisa Habari mpya wa TFF Alfred Lucas Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzia leo Aprili 27, 2016. Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS). Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri. Baraka Kizuguto Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha. Mawasiliano ya Afisa Habari,

Mbao FC ya jijini Mwanza yatangazwa kupanda Ligi Kuu ya (VPL)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League). TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo. Mbao FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo. Timu ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa Pwani. Wakati huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali ambazo zi...

Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi wa TCRA

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Ali Yahya Simba

Uongozi wa Akudo wampa Ufagio Zagreb

UONGOZI wa bendi ya Akudo Impact   unaonesha  kuwanamatumaini makubwa ya  kiongozi wa bendi hiyo Zagreb Butamu ambaye tangu aanze kuwaongoza wanamuziki  wenzake kumeonekana kuwa na mabadiliko mapya. Meneja wa bendi hiyo Ramadhani Pesambili ameliambia Jalida hili kuwa jana kuwa bendi hiyo imekuwa na mwonekano mpana zaidi hali inayoonesha kuwa  Zagreb anamudu vyema nafasi yake. kiongozi wa bendi ya Akudo Zagreb Butamu akitumbuiza jukwaani "Mpaka sasa miezi imeanza kuhesabika huku bendi ikiwa katika hatua zingine za mabadiliko hali inayofanya mashabiki kuona tofauti kubwa yenye tija katika uongozi mpya wa  Zagreb ,"alisema Rama. Rama  alisema kuwa kumekuwa na mambo muhimu katika ujio wake kiuongozi  na hivyo hali hiyo inachochea mashabiki pia kuona badiliko katika bendi. Kwa sasa bendi hiyo ambayo ni kati ya bendi zenye ushindani mkubwa nchini tangu mwishoni mwa mwaka jana inaonesha kuwa na mabaliko hayo makubwa kwa mashabiki wake na i...

Soma habari hii kutoka kwa Saleh Ally, Coruna

  MTEMBEZI ambaye anatafuta kujifunza si sawa na aliyekaa tu nyumbani akiamini vitu vitakuja na kumfuata mahali alipo.   Kila ninapopata safari hasa zinazohusiana na masuala ya soka au burudani, nimekuwa nikipenda kujifunza na wadau wa tasnia husika. Ninajua haitakuwa rahisi kila mmoja kupata nafasi anayoipata mwingine.  Ikitokea mwingine akapata nyingine, basi inakuwa rahisi kushirikiana nao kwa kuwaeleza aliona nini na kujifunza kipi ili awasaidie na wengine.  Nilipotua katika Mji wa Coruna ambao upo Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Hispania, nimejifunza mengi likiwemo moja ambalo sikuwahi hata kulisikia. Wakati tukiwa katika ziara ya kutembelea Uwanja wa Raizor unaomilikiwa na Derpotivo la Coruna waliokuwa wanatarajia kuwakaribisha Barcelona katika mechi ya La Liga, kesho yake, yaani juzi, niligundua jambo moja la ajabu kidogo kuhusiana na vyumba vya kubadilishia nguo.     tJambo hilo lilifanya niamini kweli mpira ni f...

Prima Afro Total Hair Collection yajitosa Miss dar City centre 2016

Wakati wanyange  wanaosaka kinyang'anyio cha kulitaka taji la ulimwende la   Miss Dar City centre  2016 wakiwa wameanza kukutana kuanzia mwanzo mwa wiki hii kwenye ukumbi wa Club Maisha uliopo Kijitonyama Jijini hapa es Salaam  kampuni ya  uuzaji wa nywele bandia nchini Prima Afro Total Hair Collection ambao wanapatikana  mtaa wa Narung'ombe, Kariakoo, Dar es Salaam wamejitokeza  kudhamini shindano hilo . Wauzaji hao wa nywele bandia  ambao bidhaa zao zinapatikana nchi nzima ambapo kwa djijini Dar es Salaam wanapatika katika maduka yao yaliyopo Karia Koo,wamekuwa ni wauzaji wanaojihamini kumpendezesha mwanamke  wa kisasa kuwa na mtazamo mkubwa kulingana na mwanamke anayekuwa ametumia bidhaa zao . Kujitokeza kudhamini kwa wadhamini hao  mwaka huu  maandalizi ya shindano hilo tayari yameanza katika sehemu mbali mbali  nchini  mratibu wa shindano la Miss dar City centre  2016 Nancy Jose...

Ban ambana Machar kurejea haraka Juba

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Ijumaa (22.04.2016) amemuwekea mbinyo zaidi kiongozi wa waasi nchini Sudan kusini Riek Machar kurejea mjini Juba "bila kuchelewa" na kuanza kazi katika serikali ya mpito. Machar alitarajiwa kurejea katika mji mkuu siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa makubaliano ya kisiasa yenye lengo la kumaliza vita vya miaka miwili, lakini tofauti kuhusiana na mipango ya kiusalama mjini Juba inachelewesha kurejea kwake. Ban amesema serikali ya rais Salva Kiir imekubali pendekezo la muafaka kuhusiana na matayarisho ya kurejea kwa Machar na kusema hatua hii inapaswa kusaidia kuundwa kwa haraka kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa. "Kuendelea na hali ya ushirikiano itakuwa muhimu wakati viongozi wa nchi hiyo wakianza mchakato wa kubadilisha miaka ya uharibifu uliosababishwa na mzozo huo kwa watu wa Sudan kusini," amesema katika taarifa. Mateso ya watu wa Sudan kusini Ban amemtaka Macha...

Q Chief:Aishukia QS Entertainment

Msanii mkongwe katika mziki wa bongo Q chief anaamini wingi wa wasanii wanaosimamiwa na QS Entertainment unachelewesha mipango yake kutimia. Akiongea na Enewz ya EATV, Q chief amesema label hiyo ambayo ipo chini ya QSJ Mhonda inasimamia wasanii wengi kiasi cha kuweka ugumu kwenye mipango yake kutimia. Hivi karibuni, Pia Q chief aliiambia Bongo5 kuwa bosi wake amekuwa mzito katika maamuzi mbalimbali ya kazi. label hiyo inamsimamia Q chief, Mb dog, Bushoke, ina bendi ‘QS International Band’ na pia label hii inamiliki wasanii wengine wachanga kwa lengo la kuendeleza vipaji vipya.

Rais Magufuli Azingumzia Watumishi Hewa

Rais John Magufuli juzi aliwazungumzia makada walioihama CCM wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita, alipoeleza kuwa kuondoka kwao pengine kulimsaidia kupata ushindi. Bila kutaja majina ya waliokihama chama, Magufuli alisema ni vyema wana CCM wakasahau tofauti zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo na kuganga yajayo. Rais alisema hayo kwenye mkutano na viongozi wa CCM wa mikoa na wilaya zote nchini, uliofanyika juzi Ikulu jijini Dar es Salaam. Alisema kuna mengi yalitokea wakati wa uchaguzi huo na yalikidhoofisha chama na hivyo kuna haja ya kuyasahau yaliyopita na kuangalia mbele katika kukijenga chama. “Lakini inawezekana wale walioamua kwenda kule walisaidia mimi kushinda,”alisema bila ya kufafanua. Baadhi ya wana CCM waliokihama chama hicho wakati wa uchaguzi huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kuanzia ndani ya chama hicho ni pamoja na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowasa aliyehamia Chadema, Frederick Sumaye, ambaye kwanza alitangaza kujiunga na upinz...

Hatimaye Alexis Sanchez awapoza mashabiki

IKICHEZA kwa kujiamini na kutawala mchezo, Arsenal imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom huku mashambuliaji wake, Alexis Sanchez akionyesha kiwango cha juu. Pamoja na ushindi huo Arsenal ilicheza mchezo huo ikiwa na upungufu wa mashabiki ambapo Uwanja wa Emirates haukujaa kama ilivyokawaida yake kutokana na mashabiki kususia kiaina mchezo huo kama walivyosema mapema wiki hii.Arsenal ambayo kwa ushindi huo imefikisha pointi 63 na kurejea katika nafasi ya tatu ya msimamo huo ikiishusha Manchester City iliyokuwa juu kabla ya mchezo huo wa jana usiku kwenye Uwanja wa Emirates, imerejesha matumaini ya kupambana kuwania ubingwa au nafasi mbili za juu katika mechi nne zilizosalia. Sanchez ambaye katika mechi nane zilizopita amehusika kwa katika mabao 9 ya timu yake kwa kufunga sita na kutoa asisti 3, alianza kufunga katika dakika ya 6 kisha kuongeza la pili katika dakika ya 38 kwa kupiga faulo nzuri kutoka nje ya eneo la 18 iliyojaa wavuni moja kwa moja.Matokeo hayo...

Kim Kardashian and Daughter North In Matching Braids and Choker Necklaces

Kim is back from her trip ya kusherehekea birthday ya sister wake Kourtney. For a day out with her daughter North West they decided to play dress up in matching outfits,how cool is this??? Kim wore her nude body suit with her Military over sized jacket accessorized with her sandals za chachacha ,miwani mikubwa in style and hair style ni mbili kichwa mbinjuo. North West yeye alivishwa leather shorts a nude top zilizo match her ballet flats ,hata yeye alikuwa na an over sized denim jacket Kim alomshikia . They were both spotted na same hair style za mbili kichwa /cornrows and black choker neck pieces. Do you have a daughter/s how do you play dress up????try its fun The post Mother Daughter Styles::Kim Kardashian and Daughter North In Matching Braids and Choker Necklaces appeared first on 8020Fashions Blog .

Bosi wa Bandari Aliyetumbuliwa Jipu Akutwa na Kesi ya Kujibu Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ephraim Mgawe, pamoja na aliyekuwa Naibu wake,  Hamad Koshuma, wanaokabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka wamepatikana na kesi ya kujibu. Mgawe na mwenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya China, China Communication Construction Company Limited, kwa ajili ya ujenzi wa maghati katika Bandari ya Dar es Salaam. Leo mahakama katika uamuzi wake baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka iliwaona kuwa wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yanayaowakabili na hivyo kuwataka kupanda kizimbani kujitetea, Mei 16 mwaka huu. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo alisema kwamba ameridhika kuwa upande wa mashtaka umeweza kujenga kesi dhidi ya washtakiwa hao na kuwa wana kesi ya kujibu. “Baada ya kupitia ushahidi wa  uliowasilishwa na uapnde wa mashtaka pamoja na vi...

West Brom watota kwa Arsenal waibuka na ushindi wa 2-0

ligi kuu England iliendelea usiku wa Alhamis 21 April kwa michezo mmoja ulio kati ya Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion. Mshambuliaji Alexis Sanchez ndie alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuzipasia nyavu mara mbili alianza kufunga goli la kwa katika dakika ya 6 ya mchezo kisha akifunga goli la pili kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 38. Katika mchezo huo timu ya Arsenal iliutawala kwa asilimia 71, huku West Brom wakiutawala kwa asilimia 29. Kwa ushindi huo vijana wa Profesa Arsenal Wenger, wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa kwenye nne bora baada ya kujikusanyia alama 63 katika michezo 34 waliyocheza. Arsenal wamesaliwa na michezo minne mkono kabla ya kumalizika kwa ligi kuu England msimu

Mradi wa Dart sasa kuzifanya Daladala kutoingia mijini

Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji la Dar es Salaam  zimetakiwa  kuondoka   ifikapo Mei 2 Mwaka huu ilikupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi kuweza kufanya shughuli zake kuanzia hiyo Mei 10.  Juzi, Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema mradi huo utaanza kutoa huduma kwa wakazi wa jiji hilo Mei 10. Msemaji wa mradi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Dacoboa), Sabri Mabrouk alisema wamiliki wote wa daladala walilipwa fidia ya kubadili njia. “Wamiliki wa mabasi walishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,’ ’ alisema. Mabasi hayo zaidi ya 30 ya Darts yalianza kupita kwenye njia zote za mradi huo. Changamoto kubwa inayolalamikiwa ni muingiliano wa daladala, magari binafsi, pikipiki na raia kupita bila tahadhari kwenye njia za mra...

KIWANGO SAFI CHA OSCAR JOSHUA DHIDI YA AL AHLY, HAJI MWINYI KAYASEMA HAYA…

    Mlinzi wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi amesifia kiwango cha mlinzi mkongwe Oscar Joshua wa klabu hiyo ambaye wamekuwa wakichuana kuwania nafasi katika kikosi cha kwanza, Mwinyi kwa sasa anauguza majeraha ambayo yamemuweka nje ya uwanja na kumfanya akose michezo kadhaa ikiwa ni pamoja na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly. Mwinyi amesema Joshua ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa na amekuwa akicheza kabla hata yeye (Mwinyi) hajaanza kucheza na alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wa marudiano ugenini dhidi ya Alhly. Abubar Kisandu amezungumza na mlinzi huyo wa kushoto wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambaye bado anaendea kuuguza majera yake visiwani Zanzibar akiwa amepewa mapumziko ya muda. “Kwanza mchezo ulikuwa mgumu kwasababu nyumbani tuli-draw kwahiyo ugenini mchezo ulikuwa ni wa ushindani lakini timu yetu ilicheza vizuri”, anasema Haji Mwinyi ambaye tangu atue Yanga amekuwa tishio kwa n...

Ravia:Hapata pongezi zaidi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika. Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA). CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar. Aidha Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA. Hayatou amewatakia mafanikio mema katika nafasi mpya hizo walizochaguliwa na kuahidi CAF itaendelea kuwapa ushirikiano wa maendeleo ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar.

Keys atangaza kuja na ujio mpya

Msanii wa RNB Alicia Keys ametangaza ujio wa nyimbo mpya kupitia kurasa yake mpya ya SnapChat ‘AKStreetGoddess’. Alicia amekuwa studio na producer Pharrell na Swizz Beatz akitengeneza album yake ambayo ni muendelezo wa cd yake ya mwaka 2012 ‘Girl on Fire’. Alicia Keys pia anajiunga na timu ya kipindi cha “The Voice” kama kocha wa washiriki kwenye msimu wao wa 11.

Tazama hapa shida hizi huko majuu

Baada ya rnb staa Rihanna kumbwaga mpenzi wake Travis Scott, Riri amerudisha majeshi kwa muigizaji wa filamu mkubwa duniani Leonardo DiCaprio huku bado pakiwa na tetesi kuwa anatoka na Drake. Rihanna na Leonardo DiCaprio walikuwa pamoja kwneye tamasha la Coachella Rihanna na Leonardo DiCaprio   Rihanna Na Travis   Rihanna na Drake

Umeisikia hii Da Prince ugongea mikoko kufanya matanuzi !

Newz imenasa udaku kutoka mitaani kuwa msanii wa Bongo Fleva Baraka da Prince anaongoza kwa kuazima magari ya watu na kuvimba nayo mitaani Akipiga stori na eNewz Baraka amekanusha kashfa hizo na kusema kuwa wanaosema anagongea magari ni machizi tu. Zaidi Baraka ameongeza kuwa yeye anamiliki magari zaidi ya moja na hajawahi kuendesha gari ya mtu. Pia Baraka hakuficha kuwa kwa sasa amekwisha mtambulisha msanii mwenzake Naj kwa wazazi wake kuwa ndiye mchumba wake, na amemvisha pete ya ahadi kuwa atakuwa naye milele daima. Alipoulizwa kuwa pete hiyo inamaanisha ana nia ya kumuoa Naj, Baraka alisema “Kwa hilo Mungu ndiye anayejua”.

Magazeti ya Leo Jumatano

             

Esperance yaitupa nje Azam FC

April 19 2016 wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa (CAF) klabu ya Azam FC ilishuka mjini Rades Tunisia kucheza mchezo wake wa marudiano wa Kombe la shirikishoa barani Afrika dhidi ya klabu ya   Esperance ya Tunisia . Azam FC ambao mchezo wa awali uliochezwa Chamazi Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 2-1, wamekubali kipigo cha goli 3-0 katika mchezo huo wa marudiano. Kabla ya mchezo huo Azam FC walikuwa wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze kusonga mbele. Magoli ya Esperance yalifungwa na Bguir , Jouini na Errouge . Baada ya kuondolewa katika michuano kwa klabu ya Azam FC , Tanzania inabakia na muwakilishi mmoja pekee katika michuano ya kimataifa, ambaye ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans ambayo April 20 itacheza mchezo wake wa marudiano na wenyeji wake Al Ahly .

INAFRIKA BAND 'YATISHA' NASHVILLE, TENNESSEE

Wanamuziki wa bendi ya Inafrika toka Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu Nashville jimbo la Tennessee ambapo wapo tangia March 18, 2016mpaka April 18, 2016 kwenye tamasha linaloandaliwa kila mwaka na Dolly Parton linalofanyika kwenye park iitwyo Dollywood iliyopo mjini humo. Tamasha hilo hushirikisha bendi mbalimbali kutoka mabara yote, Bara la Afrika liliwakilishwa na Inafrika Bendi kutoka Tanzania. Wanamuziki wa Inafrika Bendi wakiwa katika picha ya pamoja na Dolly Parton. Wanamuziki wa Inafrika wakipata picha ya kumbukumbu kwenye bango la Dollywood Park. Picha ya pamoja.