Winga wa manchester united Ashley Young amedai kuwa yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aendelee kutumikia kikosi hicho.
Kwa siku za hivi karibuni ameonekana kuimarisha kiwngo chake na
kufanikiwa kurejea katika kikosi cha kwanza cha mholanzi Luis Van Gaal.
Young amekuwa chachu ya matokeo mazuri ya United katika mechi sita
zilizopita na sasa anatazamiwa kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya
taifa ya England.
Young anatarajia kuongeza mkataba wa miaka mitatu na yuko tayari
kupunguziwa mshahara, huku wakala wake akijipanga kufanya mazungumzo na
Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Comments