Baada siku kadhaa kupita kwa chama kikuu cha upinzani cha Nigeria
APC kuchukua madaraka mabadiliko hayo yameonekana kuendelea kushuhudiwa
katika nchi nyingine katika nchi ya Finland Chama kikuu
cha upinzani cha CP kimeshinda uchaguzi kwa kunyakuwa asilimia 21.1 ya kura zote zilizopigwa huku chama tawala kikipata asilimia 16.5.
Kwa mujibu wa
matokeo yasiyokuwa rasmi, chama cha CP kimeshinda viti 49, SF viti 37,
SD viti 34, DG viti 15, SP viti 38, Left Party viti 12, SFP viti 9, KD
viti 5 na chama cha kujitegema kiti 1 kati ya viti 200 vya bungeni.
Mwenyekiti wa chama cha CP Juha Sipila, alitangaza ushindi wake baada ya asilimia 98.3 ya kura kuhesabiwa.
Sipila alitoa shukrani zake kwa wananchi wa Finland.
Matokeo ya chama tawala yaliwashangaza watu wengi lakini imearifiwa
kuwa Matokeo mabaya ya chama hicho yalichangiwa na kuzorota kwa uchumi
na ongezeko kubwa la ukosefu wa kazi nchini humo.Na mitandao ya habari.
Comments