Siku mbili tu zimesalia kabla ya pambano la kimataifa la ngumi kati ya mastaa wawili Manny Pacquiao na Floyd Mayweather ambao watapanda ulingoni nakutegua kitendawili cha nani mkali zaidi.
Huku watu mbalimbali wakiweka mitazamo yao juu ya nani atamshinda mwenzake pia wapo mastaa mbalimbali kama 50 cent,P Didy ambao wameweza kuweka dau la fedha kati ya mabondia hao katika Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani.
Wakati homa ya pambano hilo ikizidi kupanda huku mabondia wote kila mmoja akimtambia mwenzake, jana tuliona PManny Pacquiao alivyowasili katika mji wa Las Vegas na familia yake pamoja na wapambe wake kwa mkwara, na leo ni zamu yaFloyd Mayweather ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa MGM Grand ambao utatumika kwa pambano hilo
(KILONGE)
Mayweather
wakati anakwenda kutazama ukumbi huo ulifurika mashabiki mbalimbali
pamoja na camera za waandishi wa habarui hazikuwa mbali kuchukua tukio
zima.
Pambano
hilo linatajwa kuwa pambano la kifahari zaidi duniani na ambalo
viingilio vyake ni vikubwa ukilinganisha na mapambano mengine yaliyowahi
kufanyika duniani.
Comments