Waandamanaji wanaotaka demokrasia mjini Hong Kong
Serikali ya Hong Kong imetangaza mapendekezo kukusu kuchaguliwa kwa kiongozi wa eneo hilo mwaka 2017.
Licha ya
kushuhudiwa maandamano barabarani ya kuitisha demokrasia zaidi na
mazungumzo ya muda mrefu mipango hiyo inasalia kuwa sawa na ile
iliyotangazwa na China mwaka uliopita.
Wenyeji wa Hong Kong watawapigia kura wagombea lakini wagombea hao watahitajika kuidhinishwa na kamati kutoka China.
Wagombea
wa nafasi hiyo ni lazima wapate uungwaji mkono wa asilimia kubwa ya
kamati ya uteuzi ambayo itawajumuisha wanachama wa chama cha kikomisti.
Hata hivyo mpango huo haukubaliki na baadhi ya wapiga kura nchini Hong Kong ambao wanataka uchaguzi wa wagombea ulio huru.CHANZO:BBC (Muro)
Comments