-Atua Las Vegas kwa basi sambamba na wapambe wake akitokea Los Angeles alipokuwa akijifua
-Ataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi
-Akataa sherehe rasmi za mapokezi yake, kuandaa sherehe yake leo kwenye hoteli
-Ataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi
-Akataa sherehe rasmi za mapokezi yake, kuandaa sherehe yake leo kwenye hoteli
BONDIA
mahiri kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao (36) jana usiku ametua jijini
Las Vegas tayari kwa pambano lake la kihistoria dhidi ya Floyd
Mayweather. Pambano hilo litapigwa Mei 2, mwaka huu katika Ukumbi wa MGM
Grand uliopo Las Vegas, Marekani.
Pacquiao ametua kwa basi akiambatana na wapambe wake akitokea Los Angeles umbali wa maili 270 alipokuwa akijifua.
Bondia huyo amesema anataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi na hategemi sana kumchapa kwa knock-out (KO).
Manny
pia amekataa sherehe rasmi za mapokezi yake na kusema kuwa ataandaa
sherehe yake leo kwenye hoteli aliyofikia ya Mandalay Bay.
Rekodi:
Mayweather ameshinda mapambano yake yote 47, kati yake 26 ameshinda kwa knock-out (KO), kwenye miaka yake 19 ya ubondia wa kimataifa.
Mayweather ameshinda mapambano yake yote 47, kati yake 26 ameshinda kwa knock-out (KO), kwenye miaka yake 19 ya ubondia wa kimataifa.
Pacquiao
yeye ameshinda mapigano 57 kati ya 64 aliyopigana tangu alipoanza
mapigano ya kimataifa mwaka 1995, kati ya hayo 38 ameshinda kwa
knock-out (KO), akipoteza 5 na kutoka sare 2.
Comments