Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Eric Cantona
amebainisha kuwa mfumo na falsafa za kocha Luis Van gaal ndivyo
viliyomsaidia kuibuka na ushindi dhidi ya Manchester city siku ya
jumapili.
Wakati nyota huyo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa
United ni klabu kubwa wakati mwingine inaweza ikaanza msimu kwa kupoteza
mechi na tulidhania kuwa kwa kiwango inachoonesha itashika nafasi ya
nne au tano lakini imeonekana kuimarika zaidi na inaweza kushika nafasi
za juu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Nyota huyo aliongeza kuwa anaamini kuwa msimu ujao Manchester united
itabeba ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kulingana na falsafa za
mholanzi huyo.
Comments