Lewis Hailton
Bingwa wa dunia wa mbio za magari ya
langalanga wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton amesema yeye yupo vizuri
zaidi kiakili kuliko mchezaji mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg.
Hamilton anaamini kuwa kisaikolojia yupo juu ya Rosberg katika mapambano
ya mataji ya msimu huu.
Lewis ameyasema hayo baada ya Nico
Rosberg raia wa Ujerumani kumtuhumu mchezaji huyo kutumia mbinu za
kumdhoofisha yeye ili ashinde. ''Mara zote huwa nasema kwamba yeye ni
bora kiakili lakini nafikiri mimi nipo bora zaidi mwaka huu" alisema
Hamilton.
Rosberg alidai kuwa Hamilton ambaye ni
raia wa Uingereza alipunguza mwendo makusudi wiki iliyopita katika
shindano la China Grand Prix na kusababisha yeye kumgonga kutokea nyuma
japo mjerumani huyo amesema jambo hilo limeshapita na kufutika.CHANZO: BBC (Muro)
Comments