Umoja wa wamiliki wa mabasi ya abiria Dar es Salaam (Darcoboa) na
Usafiri wa Dar es Salaam (UDA) wameanzisha kampuni mpya ambayo
itaendesha mradi unaosubiriwa kwa hamu wa mabasi yaendayo kasi jijini
Dar es Salaam.
Kampuni hiyo, UDA Rapid Transit, imeingia mkataba wa miaka miwili na
Wakala wa DART (Mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar) ambapo kampuni hiyo
itanunua mabasi 76 yatakayofanya kazi katika mardi wa BRT.
Mradi huo unatarajiwa kuanza kufanya kazi miezi minne kuanzia sasa.
Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa DART, Bi Asteria Mlambo,
aliwakilisha upande wa serikali kwa kusaini katika hafla hiyo huku
mwenyekiti wa Simon Group amao wanaendesha UDA, Bw Robert Kisena, na
mwenyekiti wa Darcoboa Sabri Mabruki waliwakilisha UDA Rapid Transit
wakati wa kusaini makubaliano hayo ambayo yalifanyika katika ofisi za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Said Meck Sadiki.
Bw Sadiki mwenyewe na Waziri wa nchi katika ofisi za Waziri Mkuu
ambaye anahusika na Uongozi wa Mikoa na Serikali za mitaa Bi Hawa Ghasia
alishudia kutiliana saini huko.
“Huu ni ushuhuda dhahiri kwamba serikali inaweza kufanya kazi na sekta binafsi kwa ajili ya manufaa ya umma,” alisema.
Mabasi 76 yatakayonunuliwa yatakuwa ya aina mbili. Moja litakuwa na
urefu wa mita 18 ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 150 kila
mmoja na jingine litakalokuwa na urefu wa mita 12 litakuwa na uwezo wa
kubeba abiria 80 kwa mkupuo.
Chanzo: The Citizen
Comments