MANCHESTER United
inadaiwa inamtaka kwa udi na uvumba golikipa wa Tottenham, Hugo Lloris kwani
wanamuona ni mtu sahihi wa kuichezea timu hiyo kama David De Gea ataondoka.
Mpaka sasa De Gea
ameiweka njia panda Manchester United kutokana na kutosaini mkataba mpya huku
Real Madrid wakionekana kumuhitaji zaidi ili kurithi mikoba ya Iker Casillas.
Chanzo kilipasha,
golikipa huyo namba moja wa Tottenham Hotspur ambaye kwa sasa amegota miaka 28,
anataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na chaguo lake sahihi analiona ni
Manchester United.
“Lloris ndiye
mbadala sahihi wa De Gea na Manchester United wanamfuatilia kwa karibu na hata
mwenyewe anafahamu fika jambo hili,” kilipasha chanzo kimoja cha habari.
Comments