Nchi ya Niger imeanza maombolezo ya kitaifa ambapo bendera ya taifa
hilo itapepea nusu mlingoti kufatia kuuawa kwa askari wake 50 dhidi ya
wanamgambo wa Boko haram katika eneo la ziwa Chad.
Wanajeshi hao walikua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga,
katika ziwa Chad ambako walivamiwa na wanamgambo wa Kundi la kiislamu la
Boko Haram siku ya Jumamosi asubuhi katika shambulio hilo baadhi ya
wanajeshi wa Niger waliamua kutimua mbio mara baada ya kuzidiwa nguvu.
Inasemekana kuwa shambulio hilo liliendeshwa na wapiganaji zaidi ya
wapiganaji 2000 wa Boko Haram ambao walikua na zana nzito za kijeshi.
Kwa sasa kisiwa hicho cha Karamga kinashikiliwa na wanamgambo wa Boko Haram.
Comments