Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka
kwa vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika
kufikia ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu
nzuri ya vijana kupenda michongo na sio matusi Lulu aliandika hayo
katika akaunti yake ya Instagram.
“Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.
“Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”
Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.

Comments