Skip to main content

MASOGANGE ATIMULIWA SAUZ!


Muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald 'Masogange'.

Pasport ya Agness Masogange.
Sifael Paul na Imelda Mtema
HABARI ikufikie kuwa muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald 'Masogange' anadaiwa kutimuliwa nchini Afrika Kusini 'Sauzi' na sasa amekuwa akionekana Bongo akirandaranda mitaani. Muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald 'Masogange'. TUJIUNGE JOHANNESBURG

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho Masogange ni rafiki yake aliyeko maeneo ya Midland jijini Johannesburg, Sauzi, staa huyo alitimuliwa na mwenye nyumba baada ya kodi ya pango kwisha na kutakiwa kulipa jambo ambalo lilimshinda.
Ilisemekana kwamba mwanaume aliyekuwa akimpa jeuri aliyetajwa kwa jina maarufu la Said 2010 ambaye ni mfanyabiashara, Mbongo aishie jijini humo alimtosa hivyo bidada akarejea Bongo kinyemela.
KUMBE CHANZO NI TUNDA
Habari nzito zilidai kwamba chanzo cha jamaa huyo 'kumfungia vioo' Masogange ni baada ya kunasa kwenye penzi la muuza nyago mwingine wa video za wasanii wa Kibongo aliyetajwa kwa jina maarufu la Tunda.
Ilidaiwa kwamba zile mbwembwe za Masogange za kujitundika mitandaoni zilifika mwisho baada ya Said kuhamia kwa Tunda, mtoto mweupe mwenye sura ya mvuto ambaye anaonekana kwenye video za nyimbo za akina Matonya, TID 'Mnyama', Christian Bella na wengine wengi.Ilizidi kunyetishwa kwamba, awali, Tunda alikuwa Bongo lakini jamaa huyo alimtumia tiketi ya ndege na sasa anatanua naye Bondeni kwa Madiba.
UGOMVI
Ubuyu uliendelea kumwagwa kwamba, hivi karibuni Masogange na Tunda waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku wakitukanana mitandaoni bila kuanika sababu ya bifu lao.
"Kama ulikuwa unamfuatilia Masogange wiki mbili hivi zilizopita, utagundua kuna mtu alikuwa anagombana naye. Si mwingine ni huyo Tunda ambaye amemdatisha jamaa hadi akasahau kama kuna Masogange.
"Wewe fikiria, Masogange siyo mtu wa kutua Bongo kimyakimya bila kutupia picha kwenye Instagram ili kuwarusha roho wenzake. Siyo kwamba hawezi, sasa hivi yupo juu ya mawe ndiyo maana anajificha," kilisema chanzo hicho.
SUALA LA URAIA
Chanzo hicho kilipotonywa kuwa mwaka jana Masogange alitamba kuukwaa uraia wa Sauzi na kuukana wa Bongo kilisema:"Mimi nimeishi hapa South Africa (Sauzi) zaidi ya miaka mitano. Nilishaomba uraia miaka kibao sijapata hadi leo, huyo Masogange ni nani wampe uraia kwa siku mbili? Hizo fiksi tu. Kama aliomba sawa lakini hawezi kupewa uraia kirahisirahisi. Kuna process (taratibu) ndefu hadi mtu apate uraia."
MASOGANGE ATAKWENDA TENA SAUZI?
Chanzo hicho kilizidi kudadavua kuwa siyo kwamba Masogange hatakwenda tena Sauzi kwa sababu ana watu na marafiki kibao nchini humo lakini kwa sasa hana maskani ya kufikia baada ya kutimuliwa."Anaweza kwenda any time (muda wowote) lakini mpaka awe na uhakika na pa kufikia," kiliongeza chanzo hicho.
Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Masogange, alipopatikana alisomewa kila kitu 'eituzedi' ambapo aliomba chondechonde isiandikwe kwamba ametimuliwa bali yupo Bongo kwa ajili ya mapumziko.
"Jamani si kweli, waambie wahariri nipo huku (Bongo) kwa ajili ya mapumziko tu," alisema Masogange kwa kifupi.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka juzi Masogange alikamatwa Sauzi kwa msala wa madawa ya kulevya ambapo alihukumiwa kisha akalipa faini na kurejea Bongo kabla ya baadaye kutangaza kupata uraia nchini humo. CHANZO: GLP (Muro)


Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...