Mbunge
wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha
demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya
Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika
uwanja wa mazingira bora karatu mjini juzi,amewataka wananchi wa jimbo
hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura ambayo itawapa fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka
katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu (Habari
picha na Jamiiblog).
Wananchi
waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia
mkutano wa hadhara katika uwanja wa mazingira bora Karatu mjini.
Mbunge
wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa
anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kukipiga chini
Chama cha Mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha
katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi
Ikulu.
(KILONGE)
Mwenyekiti
wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha
wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura.
Diwani
wa kata ya Karatu mjini Jublate Mnyenye aonya Redio mbao zinazosambaza
habari kuwa ana mpango wa kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) ambapo amedai yeye na chama hicho ni damu damu.
Wananchi wakimshangilia mbunge wao.
Mzee Peter akijichukulia matukio mbalimbali na simu yake ya mkononi.
Wananchi wa Karatu wakiwa makini kusikiliza.
Mwananchi akieleza kero yake kwa Mbunge wake.
Jaqueline ambaye aliwakilisha wanawake akiuliza swali kwa Mbunge wake juu ya Hospitali za serikali kukosa dawa.
Mbunge
wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha
demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya
Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.
Comments