Watanzania wawili wanaoishi Afrika Kusini wameuawa kwa kile
kinachohusisha muendelezo wa hofu na chuki dhidi ya wageni ambao
umetikisa hivi karibuni.
Taarifa ya vifo imekuja baada ya Waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe, kutangaza kutoka Oman
kwamba Tanzania imeanza kuondoa raia wake kutoka Yemen ambapo kumekumbwa
na vita ya umwagaji damu baina ya majeshi ya serikali na waasi.
Nchini Afrika Kusini, mwakilishi wa Watanzani waishio nchini humo
aliiambia The Citizen jana, kwamba watu wawili wameuawa katika ghasia za
kushambulia wageni ambazo zimesababisha vifo vya watu watano kutoka
mataifa mengine na kuwakoseasha makazi maelfu katika mji wa Durban.
Bw Bonka Kusekela, mwakilishi wa Watanzania, alitaja majina ya
marehemu kama Rashid Jumanne, muuza sigara ambaye aliuawa Jumanne huko
Stenga, mtaa uliopo Durban na mwingine ni Athumani maarufu kama China
Mapepe, ambaye aliuawa Jumanne katika jiji kubwa la jimbo la
KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Kusekela, Rashid alipigwa risasi na mtu asiyejulikana
wakati akifanya biashara yake wakati Athumani, mfungwa katika gereza
kurekebisha makosa la Westville alichoma kisu hadi kufa na wafungwa
wenzake.
“Ninavyozungumza nanyi sasa tuko katika maandamano ya amani na baadhi
ya wenyeji mjini Durban kulaani mauaji haya ya kikatili lakini
tumeshapoteza Watanzania wawili mpaka sasa,” aliiambia The Citizen kwa
simu kutokea Durban.
Lakini kwa majibu ya haraka, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Elibariki Ngoyai Lowassa alisema hakuna taarifa rasmi kwamba watu wawili
wamefariki kutokana muendelezo wa ghasia dhidi ya wageni.
Akizungumza na The Citizen kutoka Afrika Kusini, hatahivyo, Bw Lowassa, alithibitisha vifo vya Watanzania wawili.
Chanzo: The Citizen
Comments