Chama Cha ACT-Wazalendo Cha Ung'uruma Singida Nakuendelea Kufungua Matawi Kikiongozwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama
hicho Anna Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha
Kintintu wilayani Manyoni mkoani Singida.
Wakazi wa Manyoni wakipiga picha na simu zao.
Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Kintintu mara baada ya kuzindua tawi la chama hicho.
Katika mazungumzo yake Zitto amesema ACT kinaweza kuunganisha
nguvu na yama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi
kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni
kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama
vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika
madaraka.
Kauli hiyo
ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe
wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi
ukombozi.
"Tumedhamiria kuleta mapinduzi
ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo
wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT-
Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na
hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu
mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi
na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi
huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari
kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao
ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Manyoni Mjini.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
Zitto Kabwe akisalimiana na wakazi wa Manyoni.
Viongozi wakiimba wimbo wa taifa.
Comments