Waziri wa
mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kushoto) na mwenzake wa Urusi
Sergei Lavrov (R) wakisubiri mkutano wao nchini Uswis Machi 29,2015
kuzungumzia mpango wa nyuklia wa Iran
Marekani
imepinga hatua ya Urusi ya kuiondolea vikwazo vya silaha Iran, huku
Urusi ikilenga kuipatia nchi hiyo mfumo wa kudhibiti makombora
ujulikanao kama S-300.
Waziri wa
mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alimpigia simu waziri mwenzake wa
Urusi, Sergei Lavrov, ambaye amesema uamuzi wa hiyari uliochukuliwa na
Urusi kuiwekea vikwazo vya silaha Iran mwaka 2010 hauhitajiki tena,
kufuatia muundo wa makubaliano wa kimataifa wa mwezi uliopita kuhusu
mpango wa Iran wa nyuklia.
Marekani
inachukulia vikwazo hivi kuwa sehemu ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa
ambavyo havitakiwi kuondolewa hadi mwishoni mwa mwezi Juni wakati
mkataba wa mwisho utakapofikiwa.
Waziri wa
Ulinzi wa Iran, Hossein Dehghan amesema uamuzi wa Urusi utasaidia
kuanzisha usalama na utulivu katika eneo hilo. Lakini Israel imekosoa
hatua hiyo.
Waandishi
wa habari wanasema Israel inahofia kuwa mfumo wa kudhibiti makombora wa
S-300 utafanya mashambulio ya anga dhidi ya taasisi za nyuklia za Iran
kuwa magumu zaidi.BBC
Comments