BONDIA asiyepigika
mpaka sasa Floyd Mayweather ametua ndani ya Las Vegas kwa ajili ya pambano lake
linalosubiriwa kwa hamu kubwa dhidi ya Manny Pacquiao linalotarajiwa kupigwa
keshokutwa (Jumapili saa 12 asubuhi kwa saa za Tanzania).
Hii ni siku moja
tu baada ya Manny Pacquiao kutua ndani ya mji huo kuelekea pambano hilo la
kihistoria lenye kuingiza fedha ndefu katika historia ya ngumi duniani.
Alipotua alianza
tambo zake na kusema ndani ya saa 48 zilizopita tayari alikuwa ameingiza dola
milioni 11 na kukiri wazi pambano hilo limemuingizia fedha nyingi zaidi katika
kipindi kifupi.
“Nimekuja Las
Vegas kwa ajili ya kazi moja tu, kumtwanga mtu, naamini kwa dhati kabisa kila
kitu kitawezekana na kuendeleza historia ya kutopigwa,” alisema.
Mayweather amekuja
na msafara wake wote pamoja na basi lake maalumu lililobeba vitu vyote muhimu
anavyovihitaji kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo.
Comments