Bondia Manny Pacquiao amekubali kupambana na Floyd Mayweather kwenye pambano la masumbwi lililopangwa kufanyika May 2.
Mpaka sasa hakuna jibu rasmi kuhusu Mayweather kukubali pambano hili
na kama atatia wino kwenye mkataba ambao imeripotiwa atalipwa dola
milioni 120 kwa pambano hilo.
Promota wa pambano hili Bob Arum amesema Manny ameshakubali na kwamba
pambano litaweka rekodi kwa kuwa pambano lenye tiketi za bei ghali
zaidi kwenye histori ya masumbwi duniani.
Pambano litafanyika kwenye ukumbi wa MGM las Vega, siti kwenye ukumbi
huo ni 15000, pesa kutoka kwenye watu wanaohudhuria ukijaa ni milioni
40, mapato ya PAY-PER-VIEW ni dola milioni 200.
Comments