Makati,
Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea
kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015.
Na RFI
Nchini
Indonesia, watu wanane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la biashara
ya madawa ya kulevya wameuawa Jumanne usiku wiki hii kwa kupigwa
risasi.
Raia saba
wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa
Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa
waliouawa. Raia mmoja kutoka Ufilipino ambaye ni miongoni mwa
waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za
mwisho.
Kama
walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo
usiku wa manane Jumanne wiki hii. Raia hao ikiwa ni pamoja na raia
wawili wa Australia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria, raia
mmoja wa Ghana na raia mmoja wa Indonesia wameuawa kwa kupigwa risasi
katika jela la kisiwa kiliyo mbali cha Nusakambangan.
Pamoja na
shinikizo mbalimbali za kimataifa na maombi kutoka kwa ndugu na jamaa
za watu hao waliokua wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa ajili ya msamaha,
Jakarta ilibakia na msimamo wake mpaka mwisho. Rais Joko Widodo, ambaye
aliingia madarakani katika majira ya joto kufuatia sehemu ya kampeni
yake ya kupambana na madawa ya kulevya, ambapo alisema kutowasamehe watu
watanojihusisha na madawa hayo ya kulevya. Utekelezaji wa adhabu kwa
watu hao waliohukumiwa ulikuwa unatarajiwa.
Katika
dakika za mwisho, mmoja kati ya watu hao waliohukumiwa kifo, mwanamke
ambaye ni raia wa Ufilipino amenusurika kuuawa, jambo ambalo
limewashangaza wengi. Rais Joko Widodo ameahirisha utekelezaji wa adhabu
ya kifo kwa raia huyo wa Ufilipino baada ya kujisalimishana kudai kuwa
alikua akijihusisha na biashara ya binadamu. Lakini uamzi huo wa
kuahirisha utekelezaji wa adhabu hiyo ni wa muda mfupi kwa raia huyo wa
Ufilipino pamoja na Serge Atlaoui, raia wa Ufaransa, ambaye aliondolewa
katika dakika za mwisho kwenye orodha ya watu ambao walikua wanatarajiwa
kuuawa.
Waziri
mkuu wa Australia Tony Abbot amelaani mauaji hayo na kuyaita ya kinyama
na amemwambia balozi wake nchini Indonesia kurudi nyumbani.
Brazil pia imelaani hatua ya kuawa kwa raia wake mmoja, huku
Mataifa ya Magharibi pamoja na Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakitoa wito kwa Indonesia kutotekeleza hatua hiyo bila mafanikio.
Indonesia imetetea uamuzi wake na kusema inapambana na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini humo.
Mataifa ya Magharibi pamoja na Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakitoa wito kwa Indonesia kutotekeleza hatua hiyo bila mafanikio.
Indonesia imetetea uamuzi wake na kusema inapambana na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini humo.
Comments