Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
MWANDISHI WETU
KUTOKANA na matukio mabaya yanayomtokea staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, shehe aliyejulikana kwa jina la Shaban Ally wa jijini Dar, ameibuka na kumuonya mwigizaji huyo kwamba kama anataka 'mabalaa' yasizidi kumuandama basi arejee kwa Mungu wake kwani anaonekana amemuacha.
Shehe huyo alifikia hatua hiyo kutokana na Wastara kuandamwa na ajali za mara kwa mara kwani hivi karibuni alianguka chooni na kabla hajakaa sawa akapata ajali ya gari na kuumia usoni.Shehe Shaban alisema staa huyo anatakiwa kumrudia Mungu kwani kawaida kwa mtu anayetokewa na majanga hayo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa amebadili aina ya maisha kutoka katika yale yanayompendeza na kuishi yale yanayomchukiza Mungu.
"Wastara anatakiwa kumrudia Mungu wake, aachane na mambo ya duniani maana katika dini ya Kiislamu, usiposwali unaweza kupatwa na majanga ya ajabu kila kukicha kama hivi yanavyomtokea yeye," alisema shehe huyo.
Akizungumza
na gazeti hili, mdau mmoja wa sanaa ya filamu ambaye hakutaka jina lake
lichorwe gazetini, alisema Wastara amebadilika kwani maisha aliyokuwa
akiishi ya kujiheshimu sana kipindi mumewe Sajuki akiwa hai ni tofauti
na sasa kwani amekuwa ni mtu wa kujiachia sana hivyo anatakiwa
kubadilika.
"Wastara
anatakiwa kubadili nyendo zake, zamani tulikuwa hatumuoni katika skendo
magazetini lakini siku hizi anatokelezea kila wakati," alisema mdau
huyo.Baada ya kupata nasaha za shehe huyo, gazeti hili lilimtafuta
Wastara ili kujua kama ni kweli ameacha kuswali au la!"Mbona naswali
sana! Mimi najua haya yanayonitokea ni majaribu tu na katika maisha
kujaribiwa kupo na hata kwenye vitabu vya dini jambo hilo limeelezewa
kwa hiyo sioni kitu kigeni," alisema Wastara.chanzo:GPL(Muro)
Comments