Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2015

Yes, nitakuwepo Zari All White Party: Huddah the boss

Ile show ya kijanja inayosubiriwa kwa hamu kutoka kwa mtoto mkali aka malkia wa East Africa,Malkia wa swaga East Africa, mwanamke mzuri kuliko wote East Africa, Mwanamke Tajiri kuliko mastaa wote East East aka muke mtarajiwa wa the big super star from East Africa Diamond platnums aitwaye zari the bosslady anaungana na bosslady mwenzie huddah the boss chick kutoka Kenya kuja kuwavuruga watoto wa Tz, ni pale pale Mlimani city, tarehe ni ile ile, unaanzaje sasa kukosa? "Ambie Rafiki yako awaambie rafiki zake kuwa tarehe 01/5 KINANUKAA!!! " (In zaris voice ).ahahahah hahah shemeji umeuaaa!! Nakupendaga ujue?

Lloris apigiwa rada MANCHESTER, England

MANCHESTER United inadaiwa inamtaka kwa udi na uvumba golikipa wa Tottenham, Hugo Lloris kwani wanamuona ni mtu sahihi wa kuichezea timu hiyo kama David De Gea ataondoka. Mpaka sasa De Gea ameiweka njia panda Manchester United kutokana na kutosaini mkataba mpya huku Real Madrid wakionekana kumuhitaji zaidi ili kurithi mikoba ya Iker Casillas. Chanzo kilipasha, golikipa huyo namba moja wa Tottenham Hotspur ambaye kwa sasa amegota miaka 28, anataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na chaguo lake sahihi analiona ni Manchester United. “Lloris ndiye mbadala sahihi wa De Gea na Manchester United wanamfuatilia kwa karibu na hata mwenyewe anafahamu fika jambo hili,” kilipasha chanzo kimoja cha habari.

Floyd Mayweather atua Las Vegas LAS VEGAS, Nevada

BONDIA asiyepigika mpaka sasa Floyd Mayweather ametua ndani ya Las Vegas kwa ajili ya pambano lake linalosubiriwa kwa hamu kubwa dhidi ya Manny Pacquiao linalotarajiwa kupigwa keshokutwa (Jumapili saa 12 asubuhi kwa saa za Tanzania). Hii ni siku moja tu baada ya Manny Pacquiao kutua ndani ya mji huo kuelekea pambano hilo la kihistoria lenye kuingiza fedha ndefu katika historia ya ngumi duniani. Alipotua alianza tambo zake na kusema ndani ya saa 48 zilizopita tayari alikuwa ameingiza dola milioni 11 na kukiri wazi pambano hilo limemuingizia fedha nyingi zaidi katika kipindi kifupi. “Nimekuja Las Vegas kwa ajili ya kazi moja tu, kumtwanga mtu, naamini kwa dhati kabisa kila kitu kitawezekana na kuendeleza historia ya kutopigwa,” alisema. Mayweather amekuja na msafara wake wote pamoja na basi lake maalumu lililobeba vitu vyote muhimu anavyovihitaji kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo.

Indonesia: watu 8 waliohukumiwa adhabu ya kifo wauawa

Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015. Na RFI Nchini Indonesia, watu wanane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya wameuawa Jumanne usiku wiki hii kwa kupigwa risasi. Raia saba wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa waliouawa. Raia mmoja kutoka Ufilipino ambaye ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za mwisho. Kama walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo usiku wa manane Jumanne wiki hii. Raia hao ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Australia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria, raia mmoja wa Ghana na raia mmoja wa Indonesia wameuawa kwa kupigwa risasi katika jela la kisiwa kiliyo mbali cha Nusakambangan. ...

Indonesia: watu 8 waliohukumiwa adhabu ya kifo wauawa

Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015. Na RFI Nchini Indonesia, watu wanane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya wameuawa Jumanne usiku wiki hii kwa kupigwa risasi. Raia saba wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa waliouawa. Raia mmoja kutoka Ufilipino ambaye ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za mwisho. Kama walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo usiku wa manane Jumanne wiki hii. Raia hao ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Australia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria, raia mmoja wa Ghana na raia mmoja wa Indonesia wameuawa kwa kupigwa risasi katika jela la kisiwa kiliyo...

SHEHE AMUONYA WASTARA

Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma. MWANDISHI WETU KUTOKANA na matukio mabaya yanayomtokea staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, shehe aliyejulikana kwa jina la Shaban Ally wa jijini Dar, ameibuka na kumuonya mwigizaji huyo kwamba kama anataka 'mabalaa' yasizidi kumuandama basi arejee kwa Mungu wake kwani anaonekana amemuacha. Shehe huyo alifikia hatua hiyo kutokana na Wastara kuandamwa na ajali za mara kwa mara kwani hivi karibuni alianguka chooni na kabla hajakaa sawa akapata ajali ya gari na kuumia usoni.Shehe Shaban alisema staa huyo anatakiwa kumrudia Mungu kwani kawaida kwa mtu anayetokewa na majanga hayo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa amebadili aina ya maisha kutoka katika yale yanayompendeza na kuishi yale yanayomchukiza Mungu. "Wastara anatakiwa kumrudia Mungu wake, aachane na mambo ya duniani maana katika dini ya Kiislamu, usiposwali unaweza kupatwa na majanga ya ajabu kila kukicha kama hivi yanavyomtok...

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND

Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance. Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane. Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora ...

Mayweather!! Hivi ndivyo alivyokwenda kukagua ukumbi wa pambano

Siku mbili tu zimesalia kabla ya pambano la kimataifa la ngumi kati ya mastaa wawili Manny Pacquiao na Floyd Mayweather ambao watapanda ulingoni nakutegua kitendawili cha nani mkali zaidi. Huku watu mbalimbali wakiweka mitazamo yao juu ya nani atamshinda mwenzake pia wapo mastaa mbalimbali kama  50 cent,P Didy  ambao wameweza kuweka dau la fedha kati ya mabondia hao katika Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani. Wakati homa ya pambano hilo ikizidi kupanda huku mabondia wote kila mmoja akimtambia mwenzake, jana tuliona  PManny Pacquiao  alivyowasili katika mji wa  Las Vegas  na familia yake pamoja na wapambe wake kwa mkwara, na leo ni zamu ya Floyd   Mayweather   ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa  MGM Grand  ambao utatumika kwa pambano hilo (KILONGE) Mayweather wakati anakwenda kutazama ukumbi huo ulifurika mashabiki mbalimbali pamoja na camera za waandishi wa ...

Mimba ya Zari, Familia ya Diamond Wadai Wanashaka na Ujauzito Huo, Kauli ya Penny na Mume wa Zari Ndio Chanzo

SHAKA! Familia ya ‘President’ wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari’ ni ya kwake au magumashi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili. TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku  hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli. “Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari. “Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho  WALITAKA ATOE MSIMAMO “Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ...

Godbless Lema Amshambulia Zitto Kabwe......Amtuhumu Kuikosesha CHADEMA Ushindi Mwaka 2010

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake mkoani Shinyanga kikidai propaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo. Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Bw. Godbless Lema, aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo. Alisema chama chao bado kipo imara na hakitagawanyika kama inavyodaiwa na Bw. Kabwe ambaye CHADEMA kilimfukuza katika chama baada ya kukisaliti hivyo kukiuka Katiba ya chama hicho. "Ndugu zangu wana Shinyanga, CHADEMA tupo imara na tutaendelea kuwa imara hadi tukamate dola na kuwakomboa Watanzania ambao wanateseka tangu tupate uhuru. "Zitto hana ubavu wa kukigawa chama chetu kama anavyofikiri na kuamini...anahangaika bure, alitaka kukiua tukamshtukia na mimi ndiye mtu wa kwanza kub...

Kwa sasa Watu wanakuna vichwa Juu ya filamu ya Rush Hour

HOLLYWOO ,India HUKO nchini India kuanzia April 23 maelezo juu ya kueleweka ujuo wa filamu mpya ya  Rush Hour toleo la nne linawafanya wadau kukuna vichwa. Picha ya billboard iliyopo mjini Hollywood toka tarehe 23 April inafanya wadau kuumiza  vichwa vyao kutokana na hali ya kuwa gumzo kubwa katika vichwa vya  habari baada ya kuonekana kuwa filamu ya Rush Hour toleo la nne inakuja kubamba upyaa. Kuhusu ukubwa wa jambo hili , kwa sasa wadau wameanza kuiona  kwenye akaunti ya instagram ya Diddy ambaye ni muigizaji na mwigizaji mwingine Byung-hun Lee, huku picha ikiwa imeambatana  na ujumbe “The Rush is back,”.

Kuna vurungu huko FB

Bjou Makifu Shamshu

Makalio ya ‘Blac Chyna’ mama wa mtoto wa rapa Tyga ni Feki

Mapaparazi wamkuwa wakiwafuatilia mastaa wa kike wenye makalio makubwa ili kujua kama feki au yakuzaliwa nayo.Watu maarufu Kim Kardashian, Nicki Minaj, Amber Rosa na Blac Chyna. Hivi karibuni picha zimesambaa za mama mtoo wa rapa Tyga kuwa umbo lake kwa nyuma [Makalio] ni feki, Blac Chyna ambaye zamani alikuwa stripper alisadikiwa kuwa alifanya upasuaji ili kuongeza makalio. Blac Chyna alikanusha tuhuma hizi nakusema makalio yake ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Kuelekea Pambano la Manny Vs Mayweather,pesa watakayolipwa,rekodi mpya ya pambano lao

Bondia Manny Pacquiao amekubali kupambana na Floyd Mayweather kwenye pambano la masumbwi lililopangwa kufanyika May 2. Mpaka sasa hakuna jibu rasmi kuhusu Mayweather kukubali pambano hili na kama atatia wino kwenye mkataba ambao imeripotiwa atalipwa dola milioni 120 kwa pambano hilo. Promota wa pambano hili Bob Arum amesema Manny ameshakubali na kwamba pambano litaweka rekodi kwa kuwa pambano lenye tiketi za bei ghali zaidi kwenye histori ya masumbwi duniani. Pambano litafanyika kwenye ukumbi wa MGM las Vega, siti kwenye ukumbi huo ni 15000, pesa kutoka kwenye watu wanaohudhuria ukijaa ni milioni 40, mapato ya PAY-PER-VIEW ni dola milioni 200.

Nyota wa R&B mwenye mpango wa kupunguza makalio yake

Wakati wanawake wengi wanafanya upasuaji kuongeza ukubwa wa makalio yao, msanii wa rnb K. Michelle amesema anampango wa kupunguza makalio yake. K Michelle aliwahi kukiri kuongeza makalio yake amemjibu shabiki twitter kuwa anapunguza makalio yake iliaweze kuigiza kwenye filamu mpya anayocheza. “ Good for you! I’m about to decrease mine for a movie ,”

RAIS ZUMA KUPITISHA SHERIA YA WATU WENYE VVU KUWEKEWA ALAMA

BAADA vurugu za wenyeji kuwashambulia wageni, Afrika Kusini imetengeneza tena 'headilines' baada ya Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma kusaini muswada ambao utawalazimu watu wote watakaogundulika kuwa na Virusi vya HIV kuwekewa alama jirani na sehemu zao nyeti. Kuanzia sasa mtu atakayepimwa na kugundulika kuwa na VVU nchini Afrika Kusini hatapewa ushauri nasaha peke yake, bali pia atachorwa tattoo kuonyesha kuwa ameathirika. "Alama hiyo itawasaidia watu wote ambao hawawezi kujizuia kufanya ngono. Kama mtu hawezi kujizuia basi itabidi kuchunguza jirani na sehemu nyeti ambapo tattoo hiyo itachorwa. Uamuzi wa kupata maambukizi ya VVU utakuwa mikononi mwa kila mtu sasa. Tunawaomba wale wote ambao wanaishi na VVU waende kwenye vituo vya afya vilivyo karibu yao waweze kuchorwa tattoo hizo." Alisema Rais Zuma baada ya kusaini mus...

Natse awataka wananchi wa Karatu kujitokeza kujiandikisha

Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini juzi,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu  la wapiga kura ambayo itawapa  fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu (Habari picha na Jamiiblog). Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa mazingira bora Karatu mjini. Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kukipiga chini Chama cha Mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni j...