Na Ali Adam, Mogadishu
Furaha zilitanda katika mitaa ya Mogadishu Jumanne (tarehe 15 Oktoba)
kwani makundi ya Wasomali waliungana na Waislamu duniani kote
kuadhimisha siku ya kwanza ya Eid al-Adha.
Wavulana wa Somalia wakicheza mieleka
katika mchanga kwenye ufukwe wa Lido huko Mogadishu kusherehekea Eid
al-Adha. [Ali Adam/Sabahi]
Mamia ya waumini walishangilia kwa kukusanyika katika msikiti wa
Isbahaysiga huko Mogadishu kuswali, ikiwa ni pamoja na Rais Hassan
Sheikh Mohamud na maofisa wengine wa nchi.
Mohamud alihutubia mkusanyiko wa waumini baada ya swala ya Eid, akituma
salamu za sikukuu kwa watu wa Somalia walio nyumbani na nje ya nchi
akiwatakia amani na maendeleo.
Rais pia alijadili hali ya usalama na kisiasa ya nchi, na kutoa wito kwa
wanachama wa al-Shabaab kukumbatia amani na kujitoa katika shughuli za
kigaidi.
"Ninawaambia vijana ambao ni sehemu ya al-Shabaab, rudini kwa watu wenu
na nchi yenu kwani hamna watu wengine nje ya watu wenu. Wakati
mtakaporudi kwa watu wenu kwa majuto makubwa na kuacha kusababisha
matatizo, watawasamehe," Mohamud alisema
Watoto wa Somalia wakiwa kwenye ufukwe wa Lido wakati wakisherehekea Eid al-Adha na familia zao [Ali Adam/Sabahi]
Kufuatia swala ya Eid, familia zilizovalia vizuri ziliingia katika mitaa
ya mji mkuu wa Somalia kushangilia na ndugu na marafiki.
Elmi Mohamed, mwenye umri wa miaka 37, ambaye alirejea nyumbani kutoka
Sweden miezi miwili iliyopita, alisema alihisi kuwa yeye ni mwenye
bahati kusherekea sikukuu ya Eid nyumbani huko Mogadishu.
Comments