Mwigulu awasihi waTanzania wa Uingereza kutumia upeo waliyonayo kulisaidia taifa zaidi kimaendeleo kuliko kuwa na ushabiki wa siasa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Mbunge wa Iramba
Magharibi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba akisisitiza Jambo katika hotuba
yake aliyoitoa hapa nchini Uingereza iliyojaa mapenzi na Tanzania zaidi
ya Itikadi na kupokelewa vyema na watanzania wengi hapa UK.
Mabadiliko hayatakuja kwa kubadilisha vyama bali ni nia zenu {Mindset) zikifanywa kuwa mpya na mapenzi ya nchi yenu.”
Katika hali iliyotajwa kuwa ni ya furaha, kutokana na changamoto
zilizokuwepo siku ya jumamosi jijini Leicester Uingereza, kijana shupavu
na “JEMBE” la kujivunia katika Taifa la Tanzania Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Taifa, na Mbunge wa Ilamba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Lameck
Nchemba akiambatana na mshauri wa Rais mheshimiwa Rajabu Luhwavi, kwa
pamoja waliweza kutoa majibu ya changamoto nyingi zinazolikabili Taifa
kwa watanzania wengi waliojitokeza katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa
na watanzania wengi kutoka maeneo mbali mbali ya Uingereza.
Ujasiri, uwazi na ukweli wa mambo ya kiutendaji katika taifa letu ndio
hasa imekuwa ni chachu na kivutio kikubwa kwa watanzania wengi
waliohudhuria mkutano huo mkubwa jiji Leicester ambapo Mh. Mwigulu
Nchemba aliweza kuweka wazi mengi ambayo serikali imeweza kuyafanya
katika upande wa Elimu, Miundo mbinu na huduma za afya kwa watanzania
pia kutoa kasoro katika maeneo yanayokuwa vikwazo katika kutoa huduma
bora.
“Nchi yetu ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya, mojawapo ya mambo
ambayo tunayafanyia kazi ni suala la uraia pacha. Ni pendekezo
lililowakirishwa na Chama Cha Mapinduzi katika baraza zake za uchangiaji
maoni ya Katiba mpya. CCM inawajali watanzania wote hivyo ikaona ni
vyema na nyinyi mlioko ughaibuni kupata fursa sawa za kimaendeleo katika
nchi yenu” alisema Mhe. Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Nchemba aliendelea na kusema kwamba nchi yetu inapita katika
kipindi cha mabadiliko. Idadi ya watanzania imeongezeka kwa kiasi
kikubwa na wengi wa ongezeko hili ni vijana ambao ni watafutaji na
wajasiliamali wengi. Kuna haja kubwa kama chama kubuni taratibu nzuri za
kimaendeleo ili kuendana na wimbi hili la ongezeko la watu.
Mheshimiwa Nchemba kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi aliwasihi watanzania
waishio Uingereza kutumia upeo (Exposure) waliyonayo katika kulisaidia
taifa kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kuliko kuwa na ushabiki wa siasa
kama ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa nyumbani na badala yake wawe
chemichemi ya mawazo ya kimaendeleo katika nchi yao.
Comments