Ni ama Jumapili au Jumananne ijayo: Mbowe amtetea Lissu, ameonewa
Rais Jakaya Kikwete ameanzisha mawasiliano na viongozi wa vyama vya
siasa vyenye hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa karibuni na Bunge kwa nia ya kuandaa
mkutano kati yake na viongozi wa vyama hivyo.
Rais Jakaya Kikwete
Taarifa Ikulu kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa mawasiliano hayo
yalianza jana, kufuatia maelekezo ya Rais Kikwete kwa Ofisi ya Katibu wa
Rais.
”Kwa mujibu wa maandalizi hayo, Ofisi ya Rais, Ikulu inaangalia
uwezekano wa kuitisha mkutano huo Jumapili ya Oktoba 13 ama Jumanne ya
Oktoba 15, mwaka huu,” ilisema sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.
Taarifa hiyo pia alisema kufuatia matukio yaliyotokea Bungeni wakati wa
kujadiliwa na kupitishwa kwa Muswada huo mwezi uliopita, na maneno na
kauli mbali mbali ambazo zimetolewa na wabunge wavyama vya upinzani na
wadau wengine kufuatia kupitishwa kwa Muswada huo na Bunge, Rais Kikwete
katika hotuba yake kwa wananchi Ijumaa iliyopita alisema hoja na kauli
za wanaopinga Muswada huo zinazungumzika kwa nia njema ya kutafuta
mwafaka katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.
Wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia na kutoka
nje wakati wa kujadili na kupitishwa kwa mudwada huo wakidai kuwa
ulikuwa na kasoro kadhaa.
Kasoro hizo ni kutoshirikishwa kwa Zanzibar, madaraka ya Rais ya kuteua
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na kuvunjwa kwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba baada ya kuwasilisha Rasimu badala ya kuendelea kuwapo hadi kura
ya maoni.
Comments