- Sura mbili za Osama Bin Laden
"ANAYEOGELEA baharini haogopi mvua." Anasema Osama Bin Laden.
Tukio la ugaidi la Westgate Nairobi linanuhusishwa pia na mtandao wa kigaidi wa Al qaida. Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya ugaidi wanapata tabu kuamini kama Al qaida inahusika moja kwa moja na tukio la Nairobi.
Ni kawaida ya Al qaida kutoa matamko ya kuhusika na ugaidi pale inapotokea. Kwenye lililotokea Nairobi, bado hazijasikika sauti rasmi na za moja kwa moja kutoka Al qaida. Yawezekana kabisa, kuwa Al Shaabab ina mahusiano ya kimtandao na Al qaida, lakini, Al Shaabab iliyopoteza nguvu nyingi yawezekana iko katika kutapatapa na kuonyesha dunia kuwa bado ni tishio.
Comments