Miili miwili iliyoungua vibaya
aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya
siku ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikawa ni ya magaidi
walioshambulia kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.
Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati
ya Bunge inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao
umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa
wanajeshi.
Mamlaka ya Kenya kwa sasa inaendelea na uchunguzi wa kisayansi wa miili hiyo.
Comments