Katika kipindi cha miaka 16 iliyopita
nchi ya Rwanda imefanikiwa kuondoa kutoka jeshini wanajeshi watoto
wapatao 3,000. Lakini wakati juhudi hizi zinaendelea Umoja wa Mataifa
unasema Kigali imekuwa ikilisaidia kundi moja la waasi kutoka Congo la
M23 kuwaandikisha watoto nchini Rwanda na kuwapeleka kuungana na waasi
wa M23 kushiriki katika mapambano Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. (HM)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments