Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013
Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na
utalii mheshimiwa Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi
wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye
mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema
mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa
mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha
kutumia nakshi(Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo
la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania
2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface
ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje
ya nchi.
Comments