Dar es Salaam. Serikali inatarajia kuandaa hati ya dharura ili
kuwezesha kufanyika kwa maboresho ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho
ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yatajadiliwa upya katika Mkutano wa
Bunge unaoanza Oktoba 29 mjini Dodoma.
Viongozi wa vyama vya siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP), Nancy Mrikaria(TLP), Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP), James Mbatia NCCR-Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba(CUF), Philip Mangula(CCM) na Dk Willibrod Slaa(Chadema)wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix
Tayari vyama vya upinzani na chama tawala vimekubaliana taratibu muhimu za kufuata ili maboresho hayo yaweze kupita ndani ya Bunge. Muswada huo haukuwa umepangwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge ndio maana itabidi iombwe hati hiyo ya dharura.
Hatua hiyo ni ushindi kwa vyama vitatu vya upinzani vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi, ambavyo vilipinga muswada huo wakati wa mkutano uliopita wa Bunge Septemba, mwaka huu.
Muswada wa sheria hiyo uliopitishwa Septemba na Bunge ulisusiwa na wabunge wa vyama hivyo wa upinzani kwa maelezo kuwa una kasoro kwenye baadhi ya vipengele.
Hata hivyo, wabunge wa CCM waliamua kuendelea na mjadala na kupitisha muswada huo kitendo ambacho kilisababisha mvutano mkubwa uliomfanya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge kumaliza tofauti zao.

Comments