Rais Jakaya Kikwete, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Aseri Msangi na watendaji wake, kuangalia namna ya kuruhusu sekta binafsi kununua tani 2,672,902 za mahindi kutoka kwa wakulima Ludewa.
Pia ametaka wakulima hao waruhusiwe kuuza mahindi yao nje ya nchi.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Njombe, katika majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo mpya.
"Kuwazuia wakulima kuuza mahindi yao nje ya nchi ni kuwatajirisha wanaokaa kwenye vizuizi na kufanya ulanguzi.
Comments