Naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa Iramba magharibi Mwigulu Nchemba alifanya ziara hivi karibuni jijini Washington Dc na alizungumza na watanzania pia alipata nafasi ya kutembelea idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA).
Katika mahojiano yake na Kipindi cha Matukio Afrika pamoja na mambo
mengine alielezea kazi za chama chake na suala la elimu nchini Tanzania
Kuhusu suala la shutuma za kushuka elimu nchini humo alisema "tatizo la
waafrika tunapima uwezo wa wanafunzi kwa kutumia lugha" aliongeza kuwa
wanafunzi wanao uwezo ila hawapati nafasi ya mafunzo ndani ya kazi yaani
nadharia kwenye maeneo ya kazi.
Aidha alipoulizwa kuhusu suala la kusafiri na mshauri wa rais amesema ni
kwa kuokoa gharama na kuwaita kwenye mkutano wa vyama katika muda wake
wa ziada na amechukuliwa kwenye mkutano wake na chama kinamgharamia kwa
yale yasiyohusisha serikali aliongeza.
Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.Inatoka kwa mdau.
Comments