Gari lilokuwa limebeba wahamiaji haramu hao likiwa katika kituo cha polisi mkaoni morogoro
Wahamiaji
haramu kutoka somalia wamekamatwa Mkoani Morogoro leo .Wahamiaji hao
waliokuwa wakisafirishwa katika gari la mizigo lilokuwa limebeba shehena
ya chokaa.
Mmoja ya wahamiaji haramu akishushwa katika gari hilo akiwa katika hali mbaya.
Kwa mujibu wa
mashuhudwa wa tukio hilo wamesema gari hilo lilekamatwa katika barabara
ya morogoro iringa katika kituo kimoja cha kujaza mafuta ambapo mhamiji
haramu aliyekuwa katika gari hilo alipokosa hewa na ndipo alipotokea
kwenye shehena wa mzigo ndipo wananchi walipomwona na kuanza kupiga
kelele na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ndipo askari wa jeshi hilo
walipofanikiwa kulikamata gari hilo na kuwakuta wahamiaji haramu wakiwa
na miokate na maji wakiwa katika hali mbaya. ambapo wanne kati yao
wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa morogoro.
Afisa wa idara ya uhamiaji akizungumzia tukio hilo.
Comments