Na BENJAMIN MASESE
HATUA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kubatilisha uamuzi wa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, uliosababisha mgomo wa malori na mabasi nchini, imeanza kuchukua mwelekeo mpya, baada ya Waziri huyo kusema anatii kile alichokieleza kiongozi wake huyo, hata kama hakuridhishwa nacho.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Bungeni mjini Dodoma, Juni 2013.
Agizo la Pinda lilikuja baada ya Magufuli, kutangaza kuanza kutumika kwa kanuni namba 7 (3) ya Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 2001, inayotaka malori yote yanayozidisha uzito uliopo ndani ya asilimia tano kupunguza mzigo, kupanga mzigo upya au kulipia uzito uliozidi mara nne ya tozo ya kawaida.
Akizungumza na RAI Jumapili kupitia kwa Katibu wake, Martyin Ntemo, Waziri Magufuli alisema licha ya agizo hilo la Waziri
Mkuu, msimamo wake ni kufanya kazi na kampuni zinazoheshimu sheria na si vinginevyo.
“Maamuzi ya Waziri Mkuu hayawezi kupingwa au kuhojiwa, natii kile kilichoelekezwa, hata kama sijaridhishwa moyoni mwangu…ila msimamo wa Wizara yangu ni kufanya kazi na kampuni zinazoheshimu sheria na si vinginevyo,” alikaririwa Magufuli.
Kauli hiyo ya Magufuli inadhihirisha wazi kwamba hajaridhishwa na agizo la Waziri Mkuu la kutoa muda wa mwezi mmoja kwa watumiaji wa malori na mabasi kuendelea kutumia sheria ya zamani, wakati ufumbuzi wa tatizo ukiwa bado unatafutwa.

Comments